Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    ARSENE WENGER YUKO TAYARI KUPOKEA LAWAMA ZA MATOKEO MABOVU LAKINI HANA MPANGO WA KUONDOKA .


    • Arsene Wenger alijiunga Arsenal mwaka 1996 akitokea klabu ya Nagoya Grampus Eight na kuipa mafanikio makubwa klabu hiyo ukiwemo ubingwa EPL wa msimu 2002/03 ambao Arsenal haikupoteza mechi yoyote .
    • Amesema aangaliwe alichokifanya ndani ya miaka 22 aliyotumikia Arsenal na kuwa hana mpango wa kuachia ngazi msimu huu kama inavyodaiwa.
    ...........................................................................................................................................................

    Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger (68) amejibu mapigo kutokana na tetesi zinazomuhusu kuachia ngazi klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu na kumpisha kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel.

    Arsene Wenger amesema anakubali lawama zote za matokeo mabaya ya klabu hiyo kwa sasa zimwendee yeye lakini akisisitiza kuwa hana mpango wa kuachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.


    Arsenal inahusishwa na taarifa kumwania kocha Thomas Tuchel ambaye inasemekana ameipiga chini ofa ya Bayern Munich msimu ujao akidai kutaka kuifundisha klabu moja kubwa barani Ulaya.

    Wenger alikaririwa na kituo cha luninga cha bEIN sports akisema 
    Tazama, unapokuwa ni mtu mzima utaweka jitihada ili ufanye vizuri kwa klabu yako na kuachana na vitu vingine vyote . miaka inayozidi kusogea ndivyo unavyozidi kukumbana na ubaguzi wa umri, ninakubali kuwa mtokeo si mazuri na inabidi nibebe lawama zote.


    Thomas Tuchel anayehusishwa kujiunga na Arsenal mwishoni mwa msimu huu.


               Tuchel alishawahi kufanya kazi na Pierre-merick Aubameyang akiwa Dortmund.
     Vitu vigumu kukabiliana navyo ni dhana ya muda gani nimekaa katika klabu na umri nilio nao lakini vitu vingine vyote ninatakiwa nikubaliane navyo kwakuwa kazi hii ni kama ya umma ambapo unatakiwa utengeneze matokeo. ninakubali kuwa nitapimwa kutokana na matokeo.
    Aliongeza Wenger.

    Arsene Wenger pia alisisitiza kuwa anataka aiweke Arsenal juu msimu huu kwenye ramani ya soka la Ulaya kwa kushinda uningwa wa Europa League.

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728