HIGHLIGHTS - MECHI YA KIRAFIKI, TAIFA STARS Vs CONGO DRC
- Taifa Stars imerejesha furaha kwa watanzania baada ya kupata ushindi mbele ya Congo DRC.
- Magoli ya Stars yamefungwa na nahodha Mbwana Samatta 74' na Shiza Kichuya 85' na kuwapa furaha Watanzania ambao wamejitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeibuka na ushindi kwa kuifunga Congo DRC katika mechi ya kirafiki iliyopigwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Magoli ya Stars yamefungwa na Nahodha Mbwana Ally Samatta dakika ya 74' na Shiza Kichuya katika dakika ya 85' ya mchezo na kupeleka furaha kwa watanzania ambao walijitokeza kwa wingi hii leo.
Congo ilitua nchini na kikosi kamili ambacho kimesheheni wachezaji nyota wanaocheza soka nje ya bara la Afrika akiwemo Yannick Bolasie anayecheza klabu ya Everton ya ligi kuu England.
Stars ilionekana kutawala mchezo kwa asilimia kubwa hasa kipindi cha pili ambapo nyota mbalimbali akiwemo Simon Msuva na nahodha Mbwana Samatta walionekana kung'ara na kuisaidia Stars kuibuka na ushindi huo.

No comments