Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    MESSI AIPAISHA BARCA KUELEKEA UBINGWA, AFIKISHA MAGOLI 600 KWA KLABU NA TIMU YA TAIFA.


    •  Fc Barcelona imeendelea kubakia kileleni mwa Laliga baada ya ushindi mwembamba dhidi ya Atletico Madrid katika dimba la Camp Nou Jumapili.
    • Bao pekee lililofungwa na Lionel Messi kwa mpira wa adhabu ndogo uliomshinda Mlinda mlango Jan Oblak na kujaa wavuni mapema kipindi cha kwanza cha mchezo. 
    • Kwa goli hilo, Messi amefikisha idadi ya magoli 600 katika ngazi ya Klabu na timu yake ya Taifa ya Argentina . 
    • Baada ya ushindi huo Barcelona imefikisha alama 69 ikifuatiwa na Atletico Madrid yenye alama 61 na Real Madrid ni ya tatu ikiwa na alama 54.

    ..................................................................................................................................................................................

    Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amefanikiwa kuifikia rekodi ya kufunga magoli 600 katika ngazi ya Klabu na timu ya Taifa kwa bao pekee alilofunga dhidi ya Atletico Madrid kwenye mchezo wa Laliga  uliopigwa katika dimba la Camp Nou Jumapili.

    Bao hilo lilitokana na kosa la Thomas Partey kumdondosha Messi karibia na lango la Atletico Madrid ndipo Barcelona walipozawadiwa adhabu ndogo ambayo Messi alitumbukiza wavuni baada ya mpira kuwavuka wachezaji na mlinda mlango licha ya kuruka .

                            Lionel Messi akipiga free-kick katika umbali wa mita 25


     
    Licha ya kuruka juu, mpira uliwavuka na kuingia golini



    Messi ameifungia Barcelona jumla ya magoli 539 huku Argentina akiifungia jumla ya magoli 61. mpaka sasa Messi ndiye mfungaji anaeongoza Laliga akiwa na mabao 24 akifuatiwa na mchezaji mwenzake wa Barcelona, Luis Suarez mwenye mabao 20 huku Cristiano Ronaldo akishika namba tatu akiwa na magoli 16.

    MCHEZO UNAOFUATA>>>>>
    Ijumaa
    Malaga   Vs   Barcelona ( Laliga )
    Estadio La Rosaleda 



     

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728