KAMUSOKO, NGOMA WAKO FITI, MZEE AKILIMALI AIOMBEA DUA YANGA.
- Jumla ya machezaji watano wamerejea katika mazoezi na wengine wamerejea kutoka kwenye matatizo ya kifamilia na wameshaanza mazoezi na klabu yao.
- Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi na Yohana Mkomola wote wameshapona majeraha yao lakini baadhi yao hawatohusika katika mchezo wa Caf Champions League Jumanne.
Kuelekea mchezo wa klabu bingwa barani Afrika Jumanne kati ya Yanga na Township Rollers ya Botswana , Yanga imepata faida kubwa kutokana na urejeo wa wachezaji wao nyota katika mazoezi tayari kabisa kwa mchezo huo.
Hayo yameelezwa na Afisa Habari msaidizi wa klabu ya Yanga Bwana Godlisten Anderson Chicharito ambaye amewataja wachezaji hao watano ambao wako tayari kucheza lakini akisisitiza kuwa jukumu la kuwapanga ni la Kocha.
Thaban Kamusoko, Yohana Mkomola, Obrey Chirwa na Juma Mahadhi wamerejea kwenye mazoezi kamili ya kikosi lakini pia Nadri Haroub "Cannavaro" ameshaejea kikosini baada ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia. Wachezaji hao wapo fiti kwa 100% na watatumika kwenye mchezo wa kesho.
Donald Ngoma, Vicent Andrew "Dante" na Hamisi Tambwe wao wamerejea lakini hawatokuwa sehemu ya mchezo wa Jumanne labda mchezo wa marudio. Mazoezi yetu ya mwisho tutafanya leo katika viwanja wa Gymkana.
Wakati huohuo Katibu wa Baraza la wazee la Klabu ya Yanga Mzee Yahya Akilimali amewataka wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo nchi nzima kuungana pamoja na kuiombea klabu yao katika mchezo huo muhimu ambao anaamini Yanga itashinda na kuwapa furaha Wanajangwani.
Mzee Yahya Akilimali (katikati) akiwa katika moja ya kikao cha klabu hiyo.
No comments