MAN CITY INAHITAJI ALAMA 12 KUNYAKUWA UBINGWA EPL.
- Manchester City imeshinda michezo 25 mpaka sasa katika Premier League ikiwa na jumla ya alama 75, wakipoteza mchezo mmoja pekee dhidi ya Liverpool mwezi January.
- Inasimama kuwa ndiyo klabu pekee iliyofunga mabao mengi mpaka sasa katika ligi, wakiwa wamefunga jumla ya mabao 83 na kuruhusu nyavu zao kutikisika mara 20 pekee.
- Kutokana na msimamo ulivyo sasa wa Ligi Manchester City inahitaji alama 12 ambazo ni sawa na michezo 4 ili kuweza kutangazwa kuwa bingwa .
Klabu ya Manchester City inaweza kutangazwa kuwa bingwa mpya wa EPL kabla ya ligi kuisha endapo watashinda michezo 4 mfululizo kutoka sasa.
Waliichapa Chelsea bao 1-0 katika dimba la Etihad Jumapili, bao lililofungwa na Bernardo Silva dakika ya 46' baada ya kupokea safi kabisa kutoka kwa nahodha David Silva na kuingia kimiani baada ya mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois kushindwa kuuokoa mpira huo akiwa chini.
Hili litakuwa ni taji la tano la ligi kuu England EPL endapo watafanikiwa kuchukua msimu huu na taji la kwanza la ligi tangu msimu wa 2013/14 walipobeba mbele ya Liverpool ambao waliongoza ligi kwa kipindi kirefu kabla ya kufanya vibaya mwishoni mwa msimu.
Endapo Manchester United akipoteza au kupata sare katika mchezo wake dhidi ya Crystal Place Jumatatu basi itawapunguzia wigo wa alama wanazozihitaji City kuelekea ubingwa msimu huu na huenda akatangazwa kuwa bingwa mpya wa EPL mapema zaidi.
Tayari Manchester City imeshinda taji la ligi ( Carabaao Cup ) baada ya kuifunga Arsenal mabao 3-0 ambalo linawafanya City kuwa na matumaini ya kushinda mataji mawili au zaidi msimu huu.
MECHI INAYOFUATA>>>
Manchester City Vs Basel ( UCL )
Uwanja wa Etihad.
No comments