Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    NKURUNZIZA AWAFUNGA WATU WAWILI WALIOMCHEZEA RAFU KATIKA MCHEZO WA SOKA




    • Rais Pierre Nkurunziza ni muumini wa Kanisa la Evangekical Christian ambaye hupendelea kusafiri na kwaya ya kanisa iitwayo" Komeza Gusenga" ikimaanisha "Kuomba bila Kuchoka" kwa lugha ya kirundi.
    • Katika kanisa hilo kuna timu ya mpira wa miguu iitwayo Haleluya Fc ambayo Rais Nkurunziza anaichezea.

    __________________________________________________________________________________________________________

    Mahakama nchini Burundi imewatia hatiani raia wawili kwa kosa la kumchezea rafu Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza katika mchezo wa soka ambao kiongozi huyo wa juu alishiriki.

    Siku ya tarehe 03 February, timu yake ya Haleluya Fc ilicheza na timu ya kutoka kaskazini mwa mji wa Kiremba.

    Ni kawaida ya timu za Burundi ambazo hucheza na timu ya Rais Nkurunziza kucheza kwa utulivu mkubwa dhidi yake na hata mara nyingine kumruhusu kufunga bao kirahisi.


    Mtazamaji mmoja ambaye alihojiwa na shirika la habari la AFP alisema.
    Timu ya Kiremba ilikuwa na raia wengi ambao ni wakimbizi wa Congo ambao hawakuwa wanajua kuwa wanacheza na kiongozi wa juu wa Burundi, Kiasi kwamba walikuwa wanamkaba mara nyingi na kusababisha kudondoka mara kwa mara.


    Baada ya mchezo kumalizika ndipo viongozi wa timu ya Kiremba Cyriaque Nkebahizi na msaidizi wake Michel Mutama wakakamatwa na kufungwa alhamisi.
     ___________________________________________________________________________________
     

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728