Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    IBRAHIMOVIC KUONDOKA MWISHONI MWA MSIMU HUU


    Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amethibitisha kuwa mshambuliaji wake ZLATAN IBRAHIMOVIC ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

    Zlatan amaerejea mazoezini hivi karibuni lakini kocha wake Jose Mourinho amesisistiza kuwa mchezaji huyo atajiunga na Klabu ya LA Galaxy ya Marekani kwakuwa ndiyo ofa iliyopo kwao kwa sasa.



    Katika msimu wake wa kwanza na Man United Ibrahimovic aliweza kufunga mabao 28 ambapo pia aliisaidia kwa kiasi kikubwa kubeba Taji la Europa League kwa kuifunga Ajax Amsterdam ya Uholanzi.

    Alipohojiwa kuhusu suala hilo Mourinho alisema " Kwa Zlatan, wote tunafikiria kuwa huu ndio msimu wake wa mwisho hapa Manchester United, ni maamuzi yake mwenyewe kama ataendelea kuwepo ama ataondoka. Nafikiri anahitaji uhuru wa kuchagua mwenyewe juu ya mustabali wake mbeleni ".

    " Ni mchezaji hodari na wa kipekee isipokuwa majeraha ndiyo yamemfanya akatishe ndoto ya kuwepo na sisi kwa misimu kadhaa hapa, ni bingwa na ananakuja na ile hali ya kuwa  " Niko tayari kwa kazi ". kwahiyo anafanya kazi kwa bidii na nina imani kuwa hiyo itamuweka katika alama nzuri ambayo itatoa majibu mazuri " Alisema Mourinho.
      

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728