Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    RATIBA, ROBO FAINALI ASFC YAANIKWA



    Kuelekea robo fainali ya Azam Sports Federation Cup  (ASFC) , ratiba yake imetolewa ambapo kutakuwa na michezo minne huku macho na masikio ya wapenzi wa soka ni katika michezo miwili .

    Mchezo wa kwanza wa robo fainali utaikutanisha Singida United na Yanga katika uwanja wa Namfua mjini Singida na hii ni kutokana na uwezo wa Singida United katika mfululizo wa Ligi kuu Tanzania Bara wakiwa katika nafasi ya nne.


    Mechi nyingine ya kuvutia ni kati ya Azam Fc ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar kutoka Manungu Turiani Mjini Morogoro. Azam imekuwa ni timu kubwa na tajiri kwa sasa nchini Tanzania lakini pia Mtibwa Sugar nayo ni klabu kongwe inayozalisha vipaji vingi vya soka kwa sasa hapa nchini. 


    Mchezo mwingine ni Tanzania Prisons dhidi ya JKT Tanzania ambayo tayari imeshapata nafasi ya kupanda ligi kuu msimu ujao huku wapiga debe wa Stand, Stand United ikivaana na Njombe Mji. 


    Mshindi wa mchezo wa Singida United na Yanga atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Tanzania Prisons na JKT Tanzania. Pia mshindi kati ya Azam Fc na Mtibwa Sugar atakutana na mshindi kati ya Stand United na Njombe Mji. 








    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728