PICHA | JUMBA LENYE THAMANI YA PAUNI 6 MILLION ATAKALOISHI NEYMAR KIPINDI ANAUGUZA JERAHA LA MGUU
Wiki mbili zilizopita kulitokea na tukio la mchezaji nyota wa PSG, Neymar Jr kuumia na kulazimika kutolewa uwanjani katika mchezo wa kombe la ligi ya Ufaransa dhidi ya Marseille .
Alisafirishwa alhamisi hii kuelekea nchini kwao Brazil akiandamana na Daktari maalum wa PSG ili kumweka chini ya uangalizi mzuri akishirikiana na madaktari wa timu ya taifa ya Brazil. Kwa taarifa za awali zilizotolewa zimeeleza kwamba mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 6 na ataukosa mchezo wa marudiano wa CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya Real Madrid katika dimba la Parc De Prince.
Taarifa pia zinaeleza amepangishwa kwenye jumba la kifahari lililo pembezoni mwa jiji la Rio de Janeiro ambalo linathamani ya pauni millioni 6 ambayo ni sawa na Sh. billioni 186.4 kwa pesa ya kitanzania. katika nyumba hiyo kutakuwamo na vyumba vinne vya kulala, Gym, Helipad, Kiwanja cha Tennis na ndege binafsi.
Zitazame picha za Hoteli hiyo inayojulikana kwa jina la MANGARATIBA PARADISE RESORT .
Neymar anatarajia kufanyiwa operesheni ya kwanza ya mguu wake jumamosi katika Hospitali ya Mater Dei mjini Belo Horizonte.
No comments