Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    "MO IBRAHIM NI MVIVU WA MAZOEZI " - PIERRE LECHANTRE



    • Kwenye mchezo wa ligi kuu , Simba dhidi ya Stand United hakuonekana Mohamed Ibrahim katika kikosi cha kwanza wala cha akiba .
    • Mchezo ambao Simba ililazimishwa sare ya 3-3 dhidi chama la wana ya Stand United katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
    ____________________________________________________________________________________

    Kocha mkuu wa klabu ya Simba, Pierre Lechantre amenukuliwa akimshutumu kiungo wake Mohamed Ibrahim kuwa ni mvivu wa mazoezi ndio sababu kubwa ya kutoonekana katika kikosi kilichocheza na Stand United ijumaa.

    kocha huyo alisema
      Tunahitaji kuwa na weledi katika klabu hii, mchezaji wako asipoonekana kwenye mazoezi siku ya kwanza, siku ya pili, siku ya tatu siwezi kukubaliana na vitu hivi .


     Nina matatizo na Mo kwasababu klabu ya soka ni kama jeshi, anafikiri Simba ni klabu ya kujiachia tuu anakuja anavyojiskia. Anakuja leo kesho hafiki anasema mkewe kapata mtoto sjui anasubiri mtoto, siwezi kukubaliana na jambo hili .

    Licha ya matatizo ya kifamilia yaliyomkuta Mo Ibrahim ya kupoteza mtoto wake pia baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu Joseph Omog , Mo hajapata nafasi ya kudumu katika kikosi hicho.

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728