VITU VYA KUVUTIA KUELEKEA MCHEZO WA ARSENAL Vs MAN CITY
Kuelekea mchezo mkali wa leo round ya pili ya ligi kuu nchini England EPL, Kocha Arsene Wenger anakutana na Pep Guardiola huku akiwa na machungu ya kulikosa taji la Carabao Cup wikiendi iliyopita ambapo Arsenal alipoteza kwa mabao 3-0.
Arsenal ya Wenger imefanikiwa kushinda michezo miwili pekee kati ya miochezo 11 ya karibuni ya Premier League huku wakitoka sare michezo mitano na kupoteza michezo minne. huu sio msimu mzuri kwa klabu ya Arsenal ambapo mpaka sasa inakamata nafasi ya sita katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 45 jambo ambalo linawapa wakati mgum kuwa na matumaini ya kumaliza nafasi nne za juu .
Endapo Arsenal watapoteza mchezo wa leo, wasiwasi wa kuendelea kuwepo kwa kocha Arsene Wenger utakuwa mkubwa kutokana na msukumo wa mashabiki wanaomtaka aondoke klabuni hapo.
Tayari kumekuwa na listi ya makocha wengi ambao wanatajwa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger endapo bodi ya wakurugenzi itamkatisha mkataba wake, baadhi ya makocha hao ni Brendan Rodgers ambaye aliwahi kuzifundisha Swansea City na Liverpool, Carlo Ancelotti pia yupo katika listi hiyo pamoja na kocha wa sasa wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Low.
Upande wa Manchester City wao wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo kutokana na staili yao ya uchezaji na mwenendo wao katika Premier League ambapo mpaka sasa wanaongoza ligi wakiwa na alama 72 wakiwaacha wapinzani wao Manchester United katika nafasi ya pili kwa tofauti ya alama 13 .
Kwa mtizamo wa kawaida kwa macho ya wengi wanaaamini kuwa Manchester City atashinda taji la Premier League msimu huu kutokana na uwezo wao wanaouonyesha katika michezo yao . Manchester City wamepoteza mchezo mmoja pekee wa Premier League dhidi ya Liverpool mapema mwezi January kwa mabao 4-3.
No comments