Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    LIVERPOOL YAPANGA KUIBOMOA TENA SOUTHAMPTON

    Liverpool yajipanga kumnasa kiungo MARIO LEMINA kutoka Southampton majira ya joto ili kuimarisha safu ya kiungo msimu ujao.

     

    Mario Lemina, mgabone ambaye ambaye anacheza kiungo cha kati katika klabu ya Southampton kiasi cha kuvivutia vilabu vikubwa katika Premier League kwenye msimu wake wa kwanza. 

    Liverpool imeonesha nia ya kumsajili kiungo huyo ambaye anaaminika kuwa atakuja kucheza pamoja na Naby Keita ambaye atajiunga na Liverpool majira ya joto kutoka RB Leipzig ya nchini Ujerumani .

    Ikumbukwe kuwa endapo Lemina atatua Anfield atakuwa ni mchezaji wa nane kusajiliwa na klabu hiyo baada ya wachezaji kama Adam Lalana, Dejan Lovren, Sadio Mane, Nathaniel Clyne na Rickie Lambert ambaye baadae aliondoka klabuni hapo  na wengine wengi. 


    Mario Lemina mwenye umri wa miaka 24 amezichezea klabu za Lorient na Marseille za Ufaransa pamoja na Juventus ya Italia ambayo alishinda kombe la Serie A msimu uliopita kabla ya kujiunga na Siuthampton.  Ni wazi kuwa kutokana na namna ya uchezaji wake ya kutumia nguvu kukaba na kupokonya mipira ataisaidia Liverpool katika eneo la katikati ya uwanja .


    Southampton imekuwa ikizalisha vipaji vingi kwa miaka kadhaa sasa na kuviuza kwa klabu mbalimbali barani ulaya.  Msimu huu imeonekana kutofanya vizuri katika Premier League , ikiwa katika nafasi ya 16 na alama 27 na pia katika mashindano ya Ulaya ambayo walitolewa katika hatua za awali za UEFA Europa League 

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728