" NAMTAKA ANTHONY JOSHUA " - DEONTAY WILDER
- Deontay Wilder amemchapa Luis Ortiz raia wa Cuba ambaye hajapigwa mchezo wowote kwenye mkanda wa WBC.
- Alimdondosha mara mbili kabla ya kumchapa kwa Knockout katika round ya 10 ya pambano hilo lililofanyika jijini New York.
Mwanandondi raia wa Marekani, Deontay Wilder amejigamba kuwa yuko tayari kupigana na bondia machachari Mwingereza, Anthony Joshua huku akijigamba kuwa hamtishi chochote baada ya kumchapa bondia wa Cuba Luis Ortiz katika round ya 10 kuwania ubingwa wa WBC.
Wilder alisema.
Nataka niweke wazi kuwa, niko tayari popote alipo Joshua apate ujumbe huu.
Anthony Joshua (28) ambaye anashikilia ubingwa wa IBF na WBA atapambana na bondia raia wa New Zealand Joseph Parker kuwania mkanda wa WBO mjini Cardiff mwishoni wa mwezi Machi.
Deontay Wilder alipata shida katika round ya 7 kutetea rekodi yake ya kutopigwa katika mapambano 40 na hatimaye kuweza kumtwanga mpinzani wake huyo katika round ya 10.
Nilipata shida mwanzo hatimaye nikarudi katika mchezo. mabingwa wa kweli mara zote hutafuta mbinu na kushinda na ndicho nilichokifanya leo.Alisema Wilder ambaye amefanikiwa kuutetea ubingwa huo kwa mara ya saba mfululizo.
Naye promota wa Anthony Joshua, Eddie Hearn alikiri kuwa pambano kati ya Wilder na Joshua linaweza kutokea endapo Joshua atamchapa Joseph Parker.
No comments