Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    LIGI YA MABINGWA ULAYA - PSG ITAMZUIA REAL MADRID KWENDA ROBO FAINALI ?.


    • Paris Saint-Germain itacheza mchezo wa Uefa Champions League dhidi ya Real Madrid usiku huu.
    • Katika mchezo wa kwanza, PSG ilipoteza kwa magoli 3-1 katika dimba la Santiago Bernabeu.
    • Endapo PSG itashindwa kufuzu hatua ya robo fainali itakuwa ni kwa mara ya pili mfululizo kwao kutolewa na timu za Hispania baada ya kutolewa na Barcelona katika hatua hii msimu uliopita.
    ................................................................................................................................................

    Kuelekea mchezo wa UEFA Champions League utakaozikutanisha PSG na Real Madrid usiku huu katika dimba la Parc de Prince jijini Paris , kumesambaa taarifa ambayo inaonyesha mashabiki wa PSG wakiwa wanapiga kelele na ngoma kuazia saa saba za usiku wa kuamkia leo karibu kabisa na Hoteli ambako Real Madrid wamefikia .

    Mashabiki hao walipanga kutibua mipango ya maandalizi ya Real kuelekea mchezo huo mkubwa ambao utatazamwa na macho ya wapenda soka wengi dunia nzima usiku huu.

     
    Wachezaji wa PSG wakiwa
     mazoezini . picha kwa hisani ya REUTERS.

     Cristiano Ronaldo na wachezji wenzake
     mazoezini. picha kwa hisani ya AP

    PSG itamkosa mchezaji wake nyota, Neymar Jr ambaye aliumia mguu wiki mbili zilizopita na sasa yupo nchini kwao Brazil akipewa matibabu chini ya uangalizi wa madaktari wa PSG na timu yake ya taifa ili aweze kucheza michuano ya kombe la dunia mwezi june.

    Kumbukumbu mbaya waliyonayo PSG katika michuano hii ni msimu uliopita ambapo walitolewa na Barcelona katika hatua ya mtoano ya 16 bora kwa  kufungwa jumla ya magoli 6-5 baada ya kushinda 4-0 nyumbani Ufaransa na baadae wakapoteza kwa kufungwa 6-1 katika dimba la Camp Nou .


    Real Madrid chini ya kocha Zinedine Zidane wanahitaji kuendeleza rekodi yao ya kuchukua taji hilo mara mbili mfululizo tangu lifanyiwe maboresho makubwa. Endapo watafanikiwa kushinda ubingwa huo msimu huu itaweka hustoria ya kushinda mara tatu mfululizo.


     


     
     

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728