Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    PICHA | UTAKAVYOKUWA UWANJA WA SPURS KUELEKEA MSIMU MPYA.



    Muonekano wa uwanja mpya wa Spurs utakavyokuwa.

    • Uwanja utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 62,000 wakiwa wameketi kwenye siti huku 42,000 kati ya siti hizo zimeshauzwa kwa mashabiki.
    • Tiketi ya bei nafuu ambayo itauzwa katika uwanja huo itagharimu pauni 795 ambayo ni ongezeko la pauni 30 dhidi ya tiketi iliyokuwa ikiuzwa White Hart Lane.
    • Na tiketi ya juu zaidi itauzwa kwa pauni 1995 ikiwa ni ongezeko la pauni 295 dhidi ya tiketi ya juu zaidi inayouzwa katika uwanja wa Wembley ambao wanautumia kama uwanja wa nyumbani.

    ........................................................................................................................................................................................................................................................

    Klabu ya Tottenham Hortspurs ya nchini Uingereza imeonyesha mpango mzima jinsi uwanja wao mpya utakavyokuwa katika msimu mpya wa ligi 2018/19 zikiwepo pamoja na picha .

    Uwanja huo unaojengwa mahali ambapo kulijengwa uwanja wa zamani wa klabu hiyo wa  White Hart Lane utakuwa na uwezo wa kubeba mashabiki takribani 62,000 na ukitarajiwa kuwa na maboresho makubwa yenye lengo la kuwafurahisha mashabiki kabla na baada ya mchezo.


    Kutakuwepo na kumbi za starehe ambako kutakuwa na maDJ wa muziki, kutakuwa na chumba maalum ambako mashabiki watakuwa wakiwauliza maswali baadhi ya wachezaji wakongwe ambao walicheza kwa mafanikio katika klabu hiyo pamoja na eneo la soko ambako kutauzwa bidhaa mbalimbali za klabu hiyo.


    Uwanja huo utakamilika mwishoni mwa msimu huu na utaanza kutumika rasmi mwanzoni mwa msimu ujao kama uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo.










    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728