YANGA YARUKA USIKU KUWAFUATA TOWNSHIP ROLLERS
Picha / Kwa hisani ya Yanga @instagram
- Yanga inashika nafasi ya pili katika ligi kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 46 sawa na Simba inayoongoza ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
- Katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afika, Yanga ilifungwa mabao 2-1 nyumbani jijini Dar es Salaam wakisubiri mchezo wa marudiano ili kuwania nafasi ya kuingia katika makundi .
Klabu ya Yanga imesafiri usiku wa jumatatu kuelekea nchini Botswana kwaajili ya kuvaana na Klbu ya Township Rollers kuwania tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Dar es Salaam kwa mabao 2-1 hali inayoufanya mchezo wa marudiano kuwa mgumu na wa muhimu kwa Yanga ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
Kabla ya kuanza safari ya kuelekea Botswana, Yanga ilicheza mchezo wa ligi dhidi ya chama la wana Stand United na kuibuka na ushindi wa nane (8) mfululizo katika ligi kwa mabao 3-1 . mabao yaliyofungwa na Ibrahim Ajib mwenye magoli 7 ya VPL mpaka sasa , Obrey Chora Chirwa na bao ambalo walijifunga mabeki wa Stand United kutokana na kazi nzuri ya Yusuph Mhilu.
Alipohojiwa katibu mkuu Bwana. Charls Boniface Mkwasa " Master" kuhusu safari hiyo ya Yanga kuelekea Botswana usiku alisema.
Ni kweli kuwa sasa hivi tunajiandaa kuondoka kuelekea Botswana, ni kutokana na safari kuwa ndefu usipaone karibu hapa ila route yake ni ndefu kwasababu ya vituo kwahiyo tunalazimika tuwahi . Pia tunapunguza gharama za usafiri kusubiri ndege nyingine wakati leo kuna ndege ambayo tunaweza kupanda na tukafika mapema na kupata muda mwingi wa kupumzika na kuzoea hali.
Endapo Yanga itafanikiwa kuiondoa Township Rollers katika hatua hii itafuzu hatua ya makundi kwa msimu wa pili baada ya msimu wa 2015/16 kutolewa kwenye hatua hiyo na Zesco iliyokuwa ikifundishwa na kocha wa sasa wa Yanga Mzambia, George Lwandamina.
No comments