Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    MAURICIO PELLEGRINO AFUNGASHWA VIRAGO SOUTHAMTON



    • Baada ya kufungwa wikiendi iliyopita 3-0 na Newcastle United ambayo inanolewa na kocha Rafa Benitez aliyefanya nae kazi akatika klabu ya Liverpool.
    • Southampton imeshinda mechi moja kati ya 17 za karibuni katika Premier League.
    • Alichaguliwa mwezi june mwaka uliopita kuchukua nafasi ya Claude Puel.
    .........................................................................................................................................................................................

    Southampton imemfuta kazi kocha Muargentina Mauricio Pellegrino baada ya muendelezo mbaya wa matokeo katika ligi huku Soton ikiwa inakamata nafasi ya 17 ikiwa na alama 28.

    Southampton imeshinda mchezo mmoja kati ya 17 ya ligi ya hivi karibuni, ni kiwango kibovu kuoneshwa na klabu hiyo katika misimu ya karibuni. Soton iko katika hali mbaya ya kushuka daraja ambapo itakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa timu hiyo kushuka tangu ilipopanda misimu mitatu iliyopita.


    Pellegrino mwenye umri wa miaka 46 aliwahi kucheza vilabu mbalimbali barani Ulaya kabla ya kuanza kufundisha soka. klabu alizozichezea ni Barcelona, Valencia, Liverpool, na Alaves.

    Kabla ya kuteuliwa kuwa kocha wa Soton alikuwa kocha wa klabu ya Derpotivo Alaves inayoshiriki katika Laliga.


    Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo katika mtandao wa twitter ilisema.
    Saints leo inathibitisha kuwa imesitisha mkataba na kocha wa kikosi cha kwanza Mauricio Pellegrino.





    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728