LIVERPOOL MBIONI KUMPA OFA YA MKATABA MPYA MO SALAH WA PAUNI 200,000 KWA WIKI.
- Liverpool wako tayari kuweka mezani ofa mpya ya mkataba kwa mshambuliaji Mohamed Salah.
- Salah amefunga 28 mpaka sasa katika ligi kuu na jumla ya mabao 36 katika mashindano yote kwenye mechi 41 alizochezea klabu hiyo.
- Japo mchezaji huyo amesisitiza kuwa ana furaha klabuni hapo lakini Liverpool haitoacha kumuongezea mkataba.
Liverpool inajipanga kumpa ofa ya mkataba mpya winga mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.
Kutokana na uwezo mkubwa anaouonesha klabuni hapo, Salah amezivutia klabu mbalimbali kubwa na tajiri barani ulaya zikiwemo Real Madrid na PSG hasa kwa uwezo wake wa kufunga magoli kwa kasi na ustadi mkubwa.
Ingawa Mo Salah (26) amekuwa mwenye furaha Anfield, lakini Liverpool inataka kumpa ofa ya mkataba mpya mwishoni mwa msimu huu ambapo atakuwa analipwa pauni 200,000 kwa wiki na kumfanya kuwa ni mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo.
Staili ya uchezaji ya mohamed Salah imewafanya wapenzi wengi wa soka kumfananisha na gwiji wa soka la Barcelona, Lionel Messi ingawa mwenyewe amekanusha taarifa hiyo kuwa halingani na Messi na kusema kuwa hivyo ni vichekesho tuu vya mitandaoni.
Alijiunga na Liverpool msimu huu akitokea Roma kwa pauni 34 million na ameonekana kucheza vizuri mpaka sasa kitu ambacho kinawafanya Liverpool kufikiria kumpa mshahara mara mbili ya pauni 90,000 anazozichukua sasa kwa wiki.
No comments