Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    KILA LA KERI YANGA NA SIMBA KIMATAIFA, TUMIENI VIZURI MECHI ZA NYUMBANI






    • Yanga Sc itacheza na klabu ya Township Rollers ya Botswana katika uwanja wa Taifa jumanne Machi 07, hatua ya mtoano ya Klabu bingwa barani Afrika.
    • Simba Sc itacheza na Al Masry kutoka Misri Jumatano Machi 08, Uwanja wa Taifa pia katika hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
    ...........................................................................................................................................................

    Simba na Yanga za Dar es Salaam ndizo klabu pekee zinazoiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa msimu huu zote zikiwa katika hatua ya pili ya mtoano ya michuano hiyo miwili huku Yanga ikituwakilisha katika Klabu bingwa Brani Afrika n Simba ikituwakilisha katika Kombe la Shrikisho.

    Timu zetu zote zimepangiwa kuanza nyumbani jambo ambalo linawapa faida kubwa wageni zaidi kuliko sisi endapo tuu wataibuka na ushindi au kupata sare ya magoli. Lakini faida tuliyonayo ni kuwa nafasi nzuri ya kuwashangaza wageni wetu kwa kushinda kwa mabao mengi kwakuwa ni mchezo wa kwanza na hawajatufahamu vizuri namna tunavyocheza zaidi ya kutuona kupitia kwenye mikanda ya video.




    Yanga na Simba inapaswa zitambue umuhimu wa mechi za nyumbani ili waweze kupigana kupata matokeo ambayo yatawasaidia katika michezo ya marudiano ugenini.

     Mfano mzuri ni mechi kati ya Real Madrid na PSG kwenye ligi ya mabingwa Ulaya ambapo kabla ya mechi ya kwanza kuchezwa mechi ilionekana ni ngumu kwa Real Madrid hasa ukizingatia mwenendo wao mbovu msimu huu katika Laliga, lakini Real Madri walitambua thamani ya kucheza uwanja wa nyumbani hasa katika mechi za mtoano na hatimaye wakafanikiwa kushinda kwa 3-1 pale Santiago Bernabeu jambo ambalo limewapunguzia mzigo kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Ufaransa.




    Watanzania wanajulikana kuwa tunapenda sana soka isipokuwa matatizo tuu ya soka letu na timu ya Taifa ndiyo yanawapinguza morali hiyo, kutokana na umuhimu wa mechi hizi watanzania hatuna budi kujitokeza uwanjani kuzipa hamasa timu zetu zifanye vizuri katika viwanja vya nyumbani .

    Kauli mbalimbali zimetolewa na viongozi wa soka kuwataka wananchi na mashabiki wa soka bila kujali vilabu vyao kuungana pamoja kuzisapoti klabu zetu japo kauli hizo zimepingwa na baadhi ya viongozi na mashabiki hasa wakihusisha suala la utani wa jadi baina ya Simba na Yanga. Lakini kiuhalisia haileti picha nzuri kuona mashabiki wa klabu fulani wa hapa kwetu wakiisapoti klabu ya nje inayocheza na  klabu ya hapahapa hoja ikiwa ni utani wa jadi.

    Katika nchi zote zilizoendelea kisoka utani na uhasama wa kimchezo unakuwepo lakini linapokuja suala la klabu moja kuliwakilisha taifa basi watu wote huungana na kuipa sapoti ili iweze kufanikiwa na hatimaye sifa zote huzieendea taifa zima wakiwemo na wale ambao si mashabiki wa timu husika.

    Mwisho nimalizie kwa kuwaomba wawakilishi wetu watambue thamani ya kucheza viwanja vya nyumbani nyuma ya mashabiki wao , pia mashabiki wote wa soka tujitokeze kwa wingi kuzisapoti timu zetu bila kujali vilabu vyetu.
    nawatakia heri Yanga na Simba katika michezo yao waibuke na ushindi na iwe furaha kwa watanzania wote.

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728