Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    WENGER APOTEZA MECHI 150 ZA EPL.


    •  Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amefikisha mechi ya 150 ya kupoteza dhidi ya Brighton & Hove Albion katika ligi kuu Uingereza EPL.
    •  Amekuwa ni kocha wa sita katika listi  ya makocha waliopoteza mechi nyingi katika ligi hiyo.
     ................................................................................................................................................................


    Kocha Arsene Wenger anazidi kupata wakati mgumu msimu huu  katika Premier League, akiwa ameshapoteza  michezo 8 mpaka sasa katika mashindano yote tangu mwaka 2018 ulivyoanza.

    Arsenal inakamata nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 45 huku ikiwa imepoteza mechi nyingine dhidi ya Brighton & Hove Albion wikiendi ambayo inaifanya kuwa ni mechi ya nne mfululizo katika mashindano yote,  ni historia mbaya kuwatokea tangu mwaka 2002.


    Shinikizo linazidi kuwa kubwa kwenye benchi la ufundi la Arsenal huku kukiwa na uwezekano mdogo kwa kocha Arsenal Wenger kuendelea kuwepo klabuni hapo msimu ujao licha ya kusaini mkataba wa miaka miwili mapema kabla ya kuanza kwa msimu huu.



    Ifuatayo ndiyo Listi ya makocha Sita ambao wanaongoza kwa kupoteza mechi nyingi katika Premier League.

                                  Harry Redknap (223)
                                  Sam Allardyce (198)
                                  David Moyes (175)
                                  Steve Bruce (173)
                                 Mark Hughes (170)
                                 Arsene Wenger (150)

    Arsenal imepangwa na AC Milan katika hatua ya mtoano ya UEFA Europa League. hiyo ndiyo nafasi pekee kwa Arsenal kuapata nafasi ya kuingia katika Champions League msimu ujao endapo atafanikiwa kuchukua ubingwa huo.

    Ni kutokana na kuwa na uwezekanao mdogo wa kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye EPL, mpaka sasa Arsenal imeshaondolewa rasmi katika mbio za kubeba taji la Premier League huku ikiwa imeachwa kwa alama 30 na Manchester City inayoongoza ligi.
     



     

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728