Header Ads

ad728
  • BREAKING NEWS

    NAHODHA WA FIORENTINA AFARIKI DUNIA AKIWA USINGIZINI HOTELINI



    • Mlinzi wa timu ya taifa ya Italia na nahodha wa Fiorentina (31), Davide Astori amefariki dunia akiwa amelala katika hotel na klabu yake.
    • Timu yake ilikua ikijiandaa kucheza mchezo wa Serie A na Udinese  siku ya Jumapili mchana.
    • Chama cha soka cha Italia kimeahirisha michezo yote iliyokuwa ifanyike jumapili kwaajili ya kutoa heshima kwa kifo hicho. 
    ........................................................................................................................................

    Nahodha wa klabu ya Fiorentina na mlinzi wa  timu ya Taifa ya Italia, Davide Astori amefariki dunia muda mchache kabla klabu yake kucheza na Udinese katika mchezo wa Serie A.

    Astori amefariki akiwa na miaka 31 na alishaichezea Italia mechi 14 katika mashindano yote huku kumbukumbu kubwa ni uwepo wake katika kikosi cha Italia kilichocheza mashindano ya FIFA Confederation Cup mwaka 2013 Brazil.


    Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji huyo hakuamka asubuhi ya jumapili katika hoteli ya La di Moret huku taarifa nyingine zikieleza kuwa alikuwa akisumbuliwa  na ugonjwa wa moyo.

    Wachezaji wenzake walimgongea mlango baada ya kuwa hapokei simu pindi alipopigiwa ndipo alipokutwa katika hali hiyo.

    Chama cha soka nchini Italia kimeahirisha michezo yote iliyokuwa ichezwe jumapili ili kutoa heshima kwa mchezaji huyo.


     
    Taarifa rasmi kutoka katika account ya  twitter ya klabu ya 
    Fiorentina ilisema.
    Fiorentina kwa mshtuko na masikitiko makubwa inatangaza kuwa nahodha wake, Davide Astori amefariki dunia.

    Klabu kadhaa za Italia na zile za ligi mbalimbali zimeonesha kuguswa na kifo hicho chenye mshtuko mkubwa .

    Astori alizaliwa katika kitongoji cha Bergamo na alianza kucheza soka katika timu ya mtaani kwake ya Pentisola kabla ya kujiunga na Academy ya AC Milan mwaka 2001.


     Davide Astori alikuwa karibuni kusaini mkataba mpya na klabu ya Fiorentina kabla ya kifo hicho kumkuta.

    _______________________________________________________________________________________________________ 
     


     

    No comments

    Post Top Ad

    ad728

    Post Bottom Ad

    ad728